-Mtangazaji wa runinga ya Citizen Willis Raburu amejaliwa mke mrembo na TUKO.co.ke iliweza kubaini haya
- Mary Ngami Raburu aliweka picha yake kwenye mitandao ya kijamii bila ya vipodozi na akavutia wafuasi wake wengi
- Kulingana na picha hizo ni wazi kwamba Raburu alibarikiwa sana kupata mke mwenye sura ya kuvutia
Mtangazaji wa runinga ya Citizen Willis Raburu alifunga pingu za maisha na mpenzi wake wa dhati Mary Ngami mwaka wa 2017 kwenye sherehe iliyohudhuriwa na watu waalikwa pekee.

Habari za harusi yake ziliwashangaza baadhi ya wafuasi wake ikizingatiwa kwamba Raburu alikuwa kwenye uhusiano mwingine wa kimapenzi na Sally Mbilu ambaye alikuwa ashamposa.
Hata hivyo, Raburu na mke wake wamekuwa wakionyesha hadharani mapenzi yao kwenye mitandao ya kijamii na kuwa tamanio kwa wapenzi wengi.

TUKO.co.ke iliweza kuzuru ukurasa wa Instagram wa Ngami na kukutana na picha za kupendeza zilizomuonyesha akiwa hapajipodoa.
Ngami alikuwa kwenye mazoezi ya kudhibiti uzani wa mwili wake alipoweka picha hizo huku akiwa ametokwa na jasho kweli kweli.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

"Napenda jinsi uso wangu unavyotoa jasho nikiwa zoezini na ninapojipanguza nahisi nikiwa safi kabisa," Ngami aliandika kwa moja ya picha zake
Ngami alidhibitisha jinsi ni mrembo hata bila ya vipodozi kama ilivyo desturi kwa wanawake wengi hasa ' Slay Queens'
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibH15f5NmpKSdp5p6uLXLpaCsZaKWr7a%2B1GaYsJ2blnqxtcKhmGalmamur7DAqKWiZZKeuaJ52Jpkr6GgpLGwxshmpZplkaOusbHNnZyzmV2gxKa4yGefraWc